Hamia kwenye habari

Kuanzia kushoto juu kwenda kulia: Jumba la Ufalme Chipangara lililoharibiwa kwa kiasi kikubwa; Jumba la Ufalme Muxungue lililoharibiwa kwa kiasi kikubwa; mafuriko katika mkoa wa Sofala

FEBRUARI 9, 2021
MSUMBIJI

Kimbunga Eloise Chasababisha Uharibifu Mkubwa Msumbiji

Kimbunga Eloise Chasababisha Uharibifu Mkubwa Msumbiji

Mahali

Mikoa ya Gaza, Inhambane, Manica, Sofala, na Zambezia

Janga

  • Januari 23, 2021, upepo mkali na mvua kubwa ilipiga katika mikoa mitano nchini Msumbiji na kufanya uharibifu mkubwa katika maeneo mengi.

Athari ambazo ndugu na dada zetu wamepata

  • Wahubiri 3 walijeruhiwa

  • Wahubiri 13 walilazimika kuhama makazi yao

Uharibifu wa mali

  • Majumba 9 ya Ufalme yameharibiwa kwa kiasi kidogo

  • Majumba 9 ya Ufalme yameharibiwa kwa kiasi kikubwa

  • Majumba 3 ya Ufalme yamepata uharibifu mkubwa

  • Nyumba 53 ziliharibiwa kidogo

  • Nyumba 41 zimeharibiwa kwa kiasi kikubwa

  • Nyumba 10 zimepata uharibifu mkubwa

Jitihada za kutoa msaada

  • Kabla ya kimbunga kuanza, ofisi ya tawi ya Msumbiji ilipendekeza kwamba wahubiri wote wanaoishi katika maeneo yaliyo hatarini wahamie maeneo salama

  • Ofisi ya tawi imeweka rasmi Halmashauri nne za Kutoa Misaada (DRC) ili kutoa msaada unaohitajika kutia ndani kuwatafutia makazi ya muda wale waliolazimika kuhama makazi yao

  • Waangalizi wa mzunguko walio katika maeneo yaliyoathiriwa wanatoa utegemezo wa kiroho na faraja kwa wahubiri

  • Jitihada zote za kutoa msaada zinafanywa kupatana na miongozo ya kujilinda dhidi ya ugonjwa wa COVID-19

Tunatazamia kwa hamu wakati ambapo Ufalme wa Mungu utakomesha majanga na maumivu ambayo yanasababisha.—Mathayo 6:10.