Hamia kwenye habari

MEI 28, 2019
MSUMBIJI

Tufani Kenneth Yapiga Eneo la Kaskazini mwa Msumbiji

Tufani Kenneth Yapiga Eneo la Kaskazini mwa Msumbiji

Aprili 25, 2019, Tufani Kenneth ilipiga kaskazini mwa Msumbiji. Hii ni tufani ya pili nchini humo baada ya kupigwa na Tufani Idai ambayo ilisababisha uharibifu mkubwa mwezi Machi. Dhoruba ya mwisho ilisababisha mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi, ikaharibu nyumba, ikasomba barabara, na hata iliharibu miundombinu yao ambayo ilikuwa dhaifu.

Wahubiri 300 hivi wanaishi katika jiji la Cabo Delgado, lakini hakuna aliyejehuriwa au kufa. Hata hivyo, nyumba 9 za ndugu zetu ziliharibiwa kabisa na zingine 16 zina hali mbaya. Kwa kuongezea, Jumba moja la Ufalme limeharibiwa kabisa na Majumba matatu yameharibiwa kwa kiwango fulani. Mwangalizi wa mzunguko wa eneo hilo, mwakilishi wa idara ya Usanifu-Majengo na Ujenzi, na ndugu wawili wanaotokea ofisi ya utafsiri walitembelea makutaniko yote yaliyoathiriwa na janga hilo na kuwasaidia na mambo waliyohitaji.

Tunasali kwa ajili ya ndugu zetu wanapomlilia Yehova, huku wakimtegemea ili awape nguvu na msaada “wakati wa taabu.”— Zaburi 46:1.