Hamia kwenye habari

AGOSTI 25, 2017
NEPAL

Mafuriko na Maporomoko ya Ardhi Yaikumba Nepal

Mafuriko na Maporomoko ya Ardhi Yaikumba Nepal

Mvua kubwa za masika zimetokeza mafuriko na maporomoko ya ardhi nchini Nepal, zikiwaacha maelfu ya watu wakiwa bila makao na zaidi ya watu 140 wamekufa. Mafuriko hayo yaliharibu barabara kuu na nyaya za umeme na hivyo kuvuruga shughuli za kutoa msaada.

Ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova nchini Japani, ambayo pia inaratibu utendaji wa Mashahidi nchini Nepal, inaripoti kwamba hakuna Mashahidi ambao walijeruhiwa au kufa wakati huo. Hata hivyo, angalau familia nne za Mashahidi zimelazimika kuhama nyumba zao, ambazo ziliharibiwa na mafuriko hayo. Mashahidi wa eneo hilo wamekuwa wakiwatunza waabudu wenzao ambao wameathiriwa.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, +1-845-524-3000

Japani: Ichiki Matsunaga, +81-46-233-0005

Nepal: Reuben Thapaliya, +977-9813469616