Hamia kwenye habari

DESEMBA 9, 2016
NEW CALEDONIA

Mafuriko na Maporomoko ya Ardhi huko New Caledonia

Mafuriko na Maporomoko ya Ardhi huko New Caledonia

Mvua kubwa sana ilinyesha katika pwani ya mashariki ya New Caledonia kuanzia Novemba 21. Mvua hiyo ilinyesha kwa saa 12 na ilikuwa na kipimo cha zaidi ya milimita 400. Mvua hiyo ilisababisha mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi ambayo yalisababisha vifo vya watu watano na kuwajeruhi watu sita; watu wengine watatu hawajulikani waliko.

Kati ya wale watu watano waliokufa, wawili walikuwa Mashahidi wa Yehova. Watoto wao wawili wenye umri mkubwa ni miongoni mwa watu wanaoripotiwa kuwa walipotea.

Siku moja baada ya msiba huo, wawakilishi wawili wa ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova ya New Caledonia walifika ili kuandaa utegemezo wa kiroho na kuandaa misaada. Zaidi ya Mashahidi 40 wenyeji walijitolea kusaidia katika kusafisha nyumba za waamini wenzao zilizokuwa zimefurika.

Baraza Linaloongoza la Mashahidi wa Yehova linasimamia kazi ya kutoa misaada wakati wa msiba likiwa katika makao yao makuu huko New York, kwa kutumia pesa zilizochangwa kwa ajili ya kazi ya Mashahidi ya kuhubiri ya ulimwenguni pote.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, +1-845-524-3000

New Caledonia: Jean-Pierre Francine, +687-43-75-00