Hamia kwenye habari

NOVEMBA 15, 2016
NEW ZEALAND

New Zealand Yakumbwa na Tetemeko la Kipimo cha 7.8 na Mengine Madogo

New Zealand Yakumbwa na Tetemeko la Kipimo cha 7.8 na Mengine Madogo

Jumatatu, Novemba 14, 2016, muda mfupi baada ya saa sita usiku, tetemeko kubwa la kipimo cha 7.8 lilitikisa Kisiwa cha Kusini cha New Zealand. Ripoti za awali zilieleza kwamba watu wawili walikufa kutokana na tetemeko hilo. Tetemeko hilo lilifuatiwa na mamia ya matetemeko madogomadogo ambayo baadhi yake yalikuwa na kipimo cha 6.0 au zaidi. Pia, lilisababisha majengo kuanguka, umeme na mawasiliano ya simu yalikatizwa, na pia liliharibu barabara, mifumo ya maji safi, na ya maji taka.

Ripoti za awali za wazee wa makutaniko ya New Zealand na ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova ya Australia zinaonyesha kwamba hakuna Shahidi hata mmoja aliyeumia au kufa katika tetemeko hilo. Mashahidi walipanga halmashauri ya kutoa msaada na kuweka kituo kwenye jiji la Christchurch, lililoko kilomita 91 hivi kusini magharibi kutoka eneo lililokuwa kitovu cha tetemeko hilo. Ingawa tetemeko hilo halikuathiri sana nyumba za Mashahidi na majengo yao ya ibada, halmashauri hiyo ya kutoa msaada inafanya kazi ya kutoa mahitaji ya dharura na mahitaji ya kiroho kwa waathiriwa wa tetemeko hilo.

Baraza Linaloongoza la Mashahidi wa Yehova ambalo ofisi zake ziko kwenye makao makuu jijini New York, linaendelea kuchunguza hali kwa umakini. Ikihitajika, litairuhusu halmashauri ya kutoa msaada itumie pesa ambazo zimechangwa kwa ajili ya kazi ya ulimwenguni pote ya kuhubiri.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, 1-718-560-5000

Australia na New Zealand: Rodney Spinks, 61-2-9829-5600