Hamia kwenye habari

Wanafunzi wenye shangwe wakiwa shuleni mjini Uli (juu) na wengine walio katika shule iliyo Ibadan (chini), Nigeria

AGOSTI 9, 2023
NIGERIA

Majengo Mapya ya Shule za Kitheokrasi Yafunguliwa Nchini Nigeria

Majengo Mapya ya Shule za Kitheokrasi Yafunguliwa Nchini Nigeria

Hivi karibuni, ofisi ya tawi ya Nigeria ilijenga majengo mapya kwa ajili ya shule mbili za kitheokrasi. Majengo hayo yatatumiwa hasa kwa ajili ya Shule ya Waeneza-Injili wa Ufalme (SKE). Katika shule iliyo mjini Uli masomo yalianza Februari 2023, na kwenye shule iliyo jijini Ibadan yalianza Juni 2, 2023. Shule ya Waangalizi wa Mzunguko na Wake Zao pia itafanyiwa hapo.

Majengo hayo yalijengwa kwenye eneo ambalo lilikuwa na Jumba la Makusanyiko. Kwenye shule zote mbili kuna darasa, maktaba, na makazi ya wanafunzi. Kila mwaka, zaidi ya ndugu na dada 500 hutuma maombi ya kuhudhuria SKE nchini Nigeria. Tunatarajia kwamba kila shule itakuwa na madarasa manne kila mwaka. Madarasa yatafanywa katika Kiingereza, Kiigbo, Kipijini (cha Afrika Magharibi), na Kiyoruba.

Juu kushoto: Shule mpya iliyo Uli, Nigeria. Kulia: Shule mpya iliyo Ibadan, Nigeria

Wanafunzi waliohitimu hivi karibuni kwenye shule ya Uli, waliandika hivi kuhusu mazingira mazuri ya shule yanayostarehesha: “Mazingira yalikuwa matulivu na mahali pa kulala palikuwa pazuri na hivyo ilikuwa rahisi kwetu kukazia fikira mambo tuliyokuwa tumejifunza na kufurahia masomo. Tulijionea jinsi ndugu na dada zetu walivyofanya kazi kwa bidii ili kutunza majengo hayo na kututunza pia na kwa sababu walitujali sana tulihisi tunapendwa.”

Tuna uhakika kwamba majengo haya mapya yatawasaidia ndugu na dada zetu nchini Nigeria ‘kutimiza kikamili huduma yao.’​—2 Timotheo 4:5.