Hamia kwenye habari

DESEMBA 2, 2016
PANAMA

Kimbunga Chakumba Amerika ya Kati

Kimbunga Chakumba Amerika ya Kati

Novemba 23, 2016, Kimbunga cha Otto kilisababisha mvua kubwa, mafuriko, na maporomoko mabaya ya ardhi nchini Kosta Rika, Nikaragua, na Panama, na kusababisha maelfu ya watu kuhama. Ripoti za awali zinaeleza kwamba hakuna Shahidi wa Yehova aliyekufa wala kujeruhiwa nchini Kosta Rika na Nikaragua. Kwa kusikitisha, nchini Panama, Shahidi mmoja wa Yehova alijeruhiwa, na wenzi fulani wa ndoa ambao ni Mashahidi walikufa kwa sababu ya maporomoko ya ardhi. Mashahidi wamefanya mipango ili kuwasaidia waathiriwa kiroho na kimwili.

Baraza Linaloongoza la Mashahidi wa Yehova, ambalo linafanya kazi kutoka kwenye makao makuu yaliyopo New York, linafuatilia hali hii kwa makini sana. Ikihitajika, litaagizahalmashauri ya kutoa msaada ya eneo hilo itumie pesa zilizochangwa kwa ajili ya kazi ya ulimwenguni pote ya kuhubiri.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, 1-845-524-3000

Kosta Rika: Pedro José Novoa Vargas, 506-8302-8499

Nikaragua: Guillermo José Ponce Espinoza, 505-8856-1055

Panama: Dario Fernando De Souza, 507-6480-3770