APRILI 12, 2023
PERU
Kimbunga Yaku Kimepiga Pwani ya Peru
Kimbunga Yaku kimepiga pwani ya kaskazini mwa Peru mwanzoni mwa mwezi wa Machi 2023. Kulikuwa na mafuriko na maporomoko ya ardhi kwa siku mbili, kisha hali ya hatari ikatangazwa katika mikoa iliyo kaskazini na iliyo kati nchini. Mafuriko hayo yameharibu nyumba, madaraja, na barabara kuu, na hivyo kufanya iwe vigumu hata zaidi kukimbia.
Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata
Hakuna ndugu au dada aliyekufa
Wahubiri 2 wamejeruhiwa
Wahubiri 106 wamepoteza makao yao
Nyumba 70 ziliharibiwa
Nyumba 130 zilipata uharibifu mdogo
Majumba 5 ya Ufalme yameharibiwa
Majumba 5 ya Ufalme yalipata uharibifu mdogo
Jitihada za Kutoa Msaada
Waangalizi wa mzunguko wanashirikiana na wazee wa makutaniko katika maeneo hayo ili kuandaa msaada wa kiroho na wa kimwili kwa ajili ya wale walioathiriwa
Halmashauri 3 za Kutoa Msaada zilianzishwa ili kuratibu kazi hiyo
Tuna uhakika kwamba Yehova anawasaidia ndugu zetu nchini Peru “[kuvumilia] kikamili kwa subira na shangwe.”—Wakolosai 1:11.