Hamia kwenye habari

MACHI 30, 2017
PERU

Peru: Mafuriko na Maporomoko ya Ardhi Yanaendelea

Peru: Mafuriko na Maporomoko ya Ardhi Yanaendelea

Mvua kubwa imesababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi katika maeneo 24 kati ya 25 nchini Peru, na ripoti zinaonyesha kwamba hali hizo zinatazamiwa kuendelea. Mvua imenyesha katika nchi hiyo na kumwaga maji zaidi ya mara 10 ya kiwango cha kawaida katika msimu wa mvua (Desemba hadi Machi). Mashahidi wa Yehova wanawasaidia waabudu wenzao, kutia ndani watu wengine walioathiriwa na janga hilo.

Zaidi ya nyumba 530 za Mashahidi wa Yehova zimeharibiwa na mafuriko hayo, kutia ndani majengo 6 ya ibada (Majumba ya Ufalme). Ripoti zinaonyesha kwamba katika mji wa Huarmey, ulioko kilomita 288 kutoka Lima, mafuriko yamewalazimisha Mashahidi wengi wapande juu ya paa za nyumba zao na hawawezi kushuka kutoka huko.

Ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova ya Peru imeanzisha halmashauri nane za kutoa msaada ili kuwashughulikia Mashahidi katika maeneo yaliyoathiriwa, kutia ndani maeneo 12 ambako serikali imetangaza hali ya hatari. Tayari halmashauri za kutoa msaada zimewapelekea waathiriwa tani 22 za chakula na zaidi ya lita 22,000 za maji ya kunywa. Tani nyingine 48 za chakula na zaidi ya lita 9,000 za maji ya kunywa zitatumwa katika majuma yanayofuata. Mamia ya Mashahidi nchini Peru wamejitolea kusaidia katika kazi ya kusafisha na kujenga upya.

Baraza Linaloongoza la Mashahidi wa Yehova linasimamia jitihada za kutoa msaada kutoka kwenye makao makuu ya ulimwenguni pote, kwa kutumia michango iliyotolewa kwa ajili ya kazi ya kuhubiri ulimwenguni pote ya Mashahidi.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, +1-845-524-3000

Peru: Norman R. Cripps, +51-1-708-9000