AGOSTI 15, 2019
POLAND
Warsaw, Poland—Kusanyiko la Kimataifa la 2019 la “Upendo Haushindwi Kamwe”!
Tarehe: Agosti 9-11, 2019
Mahali: Uwanja wa Manispaa ya Legia Warsaw na Jumba la Torwar, Warsaw, Poland
Lugha ya Programu: Kiingereza, Kipoland
Idadi ya Wahudhuriaji: 32,069
Idadi ya Waliobatizwa: 190
Idadi ya Wajumbe Kutoka Mataifa Mbalimbali: 6,892
Ofisi za Tawi Zilizoalikwa: Ulaya ya Kati, Chile, Ekuado, Finland, Ufaransa, Georgia, Hungaria, Japani, Korea, Moldova, Romania, Ukrainia, Marekani
Mambo Yaliyoonwa: Bw. Kamil Kaźmierkiewicz, meneja mkuu wa hoteli ya Four Points inayoendeshwa na hoteli ya Sheraton Warsaw Mokotów (mojawapo kati ya hoteli ambazo zilitumiwa na wajumbe), aliandika hivi: “Ushirikiano wenu ni mzuri sana—Ninatamani kuwa na wageni wengine ambao ni wenye fadhili na wenye mtazamo mzuri kama wenu. Kwa kweli ninaweza kuona kwamba mnapendana sana na mna umoja. . . . Nimevutiwa sana na mipango mizuri mliyofanya katika tukio hili.”
Pia, Bw. Kamil Lubański, mmiliki wa KL Team, kampuni ya basi iliyopewa mkataba wa kuandaa usafiri, alisema hivi: “Tangu tulipoanza kufanya kazi pamoja, nilihisi kwamba tuna ushirikiano na uhusiano mzuri pamoja na Mashahidi wa Yehova. Wana mipango na utaratibu mzuri sana. Tukio hili kubwa sana lilikuwa limepangwa na kutayarishwa vizuri. Kampuni yetu imepata pendeleo la kufanya kazi wakati wa matukio ya kifahari, serikalini na imefanya kazi katika matukio mengi nchini kote na katika nchi nyingine za Ulaya. Hata hivyo, ni nadra sana kukutana na mteja ambaye amejitayarisha vizuri na aliye na mipango mizuri. Kwa ufupi, madereva na wafanyakazi wengine wana mambo mazuri tu ya kusimulia kuhusiana na jinsi wanavyoshughulika na Mashahidi wa Yehova. Tunatumaini kwamba wakati ujao tutapata fursa ya kuwahudumia tena.”
Wajumbe wakikaribishwa kwa furaha kwenye uwanja wa ndege
Wahudhuriaji wakiingia uwanjani siku ya Ijumaa asubuhi
Mwonekano kutoka juu wa uwanja wa kusanyiko wa Manispaa ya Legia Warsaw
Ndugu Gerrit Lösch wa Baraza Linaloongoza akitoa hotuba ya mwisho siku ya Ijumaa jioni
Wahubiri watatu wakibatizwa siku ya Jumamosi
Ndugu na dada wakisikiliza kwa makini programu ya kusanyiko
Wajumbe wakiwa wamevaa mavazi ya kitamaduni wanapiga picha nje ya uwanja wa kusanyiko
Watumishi wa wakati wote waliohudhuria kusanyiko hilo wakiimba wimbo wa mwisho pamoja na wahudhuriaji wengine siku ya Jumapili
Kikundi cha dada vijana wakiwatumbuiza wajumbe wakati wa tafrija ya jioni
Ndugu na dada wakicheza dansi ya kitamaduni ya Kipoland wakati wa tafrija ya jioni