SEPTEMBA 21, 2017
PUERTO RIKO
Ripoti za Awali Baada ya Kimbunga Maria
Jumatano, Septemba 20, 2017, Kimbunga Maria, kimbunga cha tano kwa uharibifu kuwahi kupiga Marekani, kilisababisha uharibifu mkubwa nchini Puerto Riko. Kwa sababu hiyo, kisiwa chote hicho hakikuwa na umeme, na serikali imeweka marufuku ya kusafiri baada ya saa 12:00 jioni.
Kulingana na ripoti tulizopata hakuna ndugu aliyejeruhiwa au kufa. Kazi ya kutoa msaada imeanza. Akina ndugu watatumia Jumba la Ufalme ambalo halijaathiriwa kuwa makao na eneo la kusambazia vitu.
Majengo ya Betheli yaliyoko San Juan yaliathiriwa kidogo. Ndugu wote huko wako salama na hakuna aliyejeruhiwa. Kwa sasa, hawana Intaneti na jenereta inatumiwa kuzalisha umeme.
Tuna uhakika kwamba ndugu zetu watafarijiwa na jitihada za tengenezo la Yehova za kutoa msaada.—2 Wakorintho 1:3
Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:
David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1-845-524-3000