MEI 12, 2023
SUDAN
Mapigano Makali Yaendelea Nchini Sudan
Aprili 15, 2023, mzozo ulizuka baina ya vikundi viwili vyenye silaha Khartoum, mji mkuu wa Sudan. Ripoti za habari zinaonyesha kwamba mzozo huo umesababisha vifo vya watu zaidi ya 600 huku wengine 5,000 wakiwa wamejeruhiwa.
Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata
Hakuna ndugu au dada yetu aliyejeruhiwa au kufa
Karibu wahubiri 318 wamelazimika kuhama makao yao. Baadhi yao wamekimbilia nchi jirani na wamefika salama
Kwa muda fulani watu 8 hakuweza kuondoka katika sehemu yao ya kazi na watoto 5 hakuweza kuondoka shuleni. Kwa sasa wote wameungana tena na familia zao
Jitihada za Kutoa Msaada
Wazee wa eneo hilo wanawategemeza kiroho wahubiri walioathiriwa
Halmashauri za Kutoa Msaada zimewekwa rasmi nchini Sudan na katika nchi jirani ili kusimamia jitihada za kutoa msaada na pia kuandaa mahitaji mbalimbali
Tutaendelea kusali kwa ajili ya ndugu zetu ambao maisha yao yamevurugwa na machafuko yanayoendelea tukisubiri kwa hamu wakati unaokuja ambapo “amani itakuwa nyingi.”—Zaburi 72:7.