Hamia kwenye habari

FEBRUARI 9, 2018
TAIWAN

Tetemeko la Ardhi Laikumba Taiwan

Tetemeko la Ardhi Laikumba Taiwan

Usiku wa Jumanne, Februari 6, tetemeko la ardhi lenye kipimo cha 6.4 lilitokea karibu na pwani ya mashariki ya Taiwan. Ripoti za habari zinaonyesha kwamba watu 6 hivi wamekufa na zaidi ya 250 kujeruhiwa. Watu 76 bado hawajulikani walipo.

Hakuna mhubiri aliyekufa au kujeruhiwa wakati wa tetemeko hilo la ardhi. Hata hivyo, jengo la ofisi ya utafsiri ya Amis (lugha ya kienyeji nchini Taiwan) na Jumba la Ufalme katika eneo la Hualien yaliharibiwa. Hualien ni mojawapo ya maeneo yaliyoathiriwa vibaya zaidi. Isitoshe, jengo ambamo baadhi ya washiriki wa kikundi cha utafsiri waliishi liliharibiwa sana hivi kwamba wakalazimika kuhama. Akina ndugu wa eneo hilo waliandaa mahali pa muda pa kulala kwa ajili ya wale walioathiriwa, na ofisi ya tawi ya Taiwan inasaidia kuandaa mahitaji mengine.

Tunasali kwamba ndugu na dada zetu walioathiriwa watapata amani ya akili wakati wa kipindi hiki chenye msukosuko, na kwamba ndugu waliokabidhiwa jukumu la kuwatunza watathibitika kuwa “kama mahali pa kujificha kutokana na upepo.”—Isaya 32:2.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, +1-845-524-3000

Taiwan: Chen Yongdian, +886-3-477-7999