Hamia kwenye habari

MACHI 19, 2021
TAJIKISTAN

Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu Yaomba Hatua za Pekee Zichukuliwe Kumhusu Ndugu Shamil Khakimov

Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu Yaomba Hatua za Pekee Zichukuliwe Kumhusu Ndugu Shamil Khakimov

Machi 19, 2021, Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu (CCPR) iliiomba nchi ya Tajikistan ichukue hatua mara moja kulinda afya ya Ndugu Shamil Khakimov mwenye umri wa miaka 70. Ndugu yetu ambaye ni mgonjwa alifungwa Februari 2019 kwa sababu ya kushiriki utendaji wa kidini kwa amani. CCPR imeomba kwamba wenye mamlaka nchini Tajikistan wamhamishie Ndugu Khakimov kwenye kituo maalumu cha afya na kwamba aachiliwe na kupewa kifungo cha badala wakati ambapo kesi yake inasubiri kusikilizwa na CCPR.