Hamia kwenye habari

JANUARI 7, 2021
TAJIKISTAN

Mahakama ya Kijeshi ya Tajikistan Yamhukumu Ndugu Rustamjon Norov Miaka Mitatu na Nusu Gerezani

Mahakama ya Kijeshi ya Tajikistan Yamhukumu Ndugu Rustamjon Norov Miaka Mitatu na Nusu Gerezani

Januari 7, 2021, mahakama ya kijeshi nchini Tajikistan ilimhukumu Ndugu Rustamjon Norov miaka mitatu na nusu gerezani kwa kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri.

Kabla tu ya uamuzi kutolewa, Rustamjon alipewa nafasi ya kuzungumza mbele ya mahakama. Kwa ujasiri alinukuu mistari kadhaa ya Biblia akieleza sababu yake ya kukataa utumishi wa kijeshi. Pia alieleza kilichomsaidia kuendelea kuwa imara.

Alinukuu Wafilipi 4:13: “Kwa mambo yote nina nguvu kupitia yule anayenipa nguvu.” Alisema hivi pia: “Katika kipindi hiki chote, nimehisi Mungu wangu, Yehova, akiwa pamoja nami na akinipa nguvu ili nisikate tamaa au kuvunjika moyo, niendelee kuwa na furaha na shangwe, na kuendelea kutabasamu. Ninamshukuru sana, na ninajivunia kumtumikia nikiwa mmoja wa Mashahidi wake.”