Hamia kwenye habari

SEPTEMBA 22, 2021
TAJIKISTAN

Ndugu Rustamjon Norov Ameachiliwa Kutoka Gerezani Nchini Tajikistan

Ndugu Rustamjon Norov Ameachiliwa Kutoka Gerezani Nchini Tajikistan

Septemba 21, 2021, Ndugu Rustamjon Norov aliachiliwa kutoka gereza la mji wa Yavan, Tajikistan. Amekuwa kizuizini tangu Oktoba 2020 kwa kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri. Alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu na nusu, lakini akaachiliwa mapema kwa sababu ya sheria mpya ya msamaha iliyoanza kutumika mapema mwezi huu.