Hamia kwenye habari

OKTOBA 2, 2019
TAJIKISTAN

Serikali ya Tajik Yamhukumu Ndugu Shamil Khakimov Mwenye Umri wa Miaka 68 Kifungo Cha Miaka Saba na Nusu Gerezani.

Serikali ya Tajik Yamhukumu Ndugu Shamil Khakimov Mwenye Umri wa Miaka 68 Kifungo Cha Miaka Saba na Nusu Gerezani.

Septemba 10, 2019, Mahakama ya jiji la Khujand lililo Tajikistan limemhukumu Ndugu Shamil Khakimov kifungo cha miaka saba na nusu gerezani kwa kosa la kueleza watu wengine imani yake tu. Mashahidi wa Yehova wamekata rufaa mahakamani.

Mateso haya ya Ndugu Khakimov yalianza mapema mwaka 2019. Februari 26, wenye mamlaka walipomkamata Shamil mwenye umri wa miaka 68, kwa tuhuma za “kuchochea chuki ya kidini.” Baadaye, mahakama ilimweka mahabusu, na kumwongezea muda wa kukaa huko kwa miezi sita. Ndugu Khakimov amevumilia yote haya licha ya kuwa na tatizo la shinikizo la damu na wakati huohuo akiuguza kidonda chake baada ya upasuaji aliofanyiwa.

Hii ni mara ya kwanza kwa Shahidi wa Yehova kufungwa Tajikistan tangu mwaka 2017 ambako Daniil Islamov mwenye umri wa miaka 18 alihukumiwa kifungo cha miezi sita kwa kukataa kuvaa mavazi ya kijeshi. Sasa, Tajikistan ni moja ya nchi tano zilizofunga Mashahidi wa Yehova gerezani. Nchi nyingine nne ni Eritrea, Urusi, Singapore, na Turkmenistan.

Tunasali kwamba Yehova aendelee kumtegemeza Ndugu Khakimov kwa kila namna ili avumilie jaribu hili.—Waroma 15:5.