JANUARI 26, 2022
TONGA
Mlipuko wa Mlima wa Volkano na Tsunami Zasababisha Madhara Nchini Tonga
Januari 15, 2022, tsunami kubwa ilipiga kisiwa cha Tonga baada ya mlima wa volkano ulio chini ya maji kulipuka kwenye Bahari ya Pasifiki. Athari zake zilisikika hadi Amerika Kusini na Japani. Majivu na mafuriko yamesababisha madhara katika eneo kubwa la Tonga, na mawasiliano yamekatizwa.
Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata
Hakuna ndugu au dada aliyejeruhiwa
Jitihada za Kutoa Msaada
Halmashauri ya Kutoa Msaada ilianzishwa
Akina ndugu wanawasaidia wale walioathiriwa kuondoa majivu kwenye paa zao kwa kuwa michirizi huwasaidia kukinga maji ya kunywa
Jitihada zote za kutoa msaada zinafanywa kupatana na miongozo ya usalama ya COVID-19
Akina ndugu wamerudia ratiba ya kiroho upesi na wanaongoza mikutano kwa ukawaida. Tunajua kwamba Yehova atathibitika kuwa “msaidizi . . . na mfariji” kwa ndugu na dada zetu walioathiriwa na janga hilo.—Zaburi 86:17.