Hamia kwenye habari

MACHI 20, 2019
TURKMENISTAN

Bahram Hemdemov Aachiliwa

Bahram Hemdemov Aachiliwa

Februari 13, 2019, Bahram Hemdemov, mwenye umri wa miaka 55, aliachiliwa kutoka gerezani nchini Turkmenistan baada ya kutumikia kifungo cha miaka minne katika gereza la Seydi (LB-E/12). Sasa ameungana tena na mke wake, Gulzira, na watoto wao wanne. Bw. Hemdemov alikamatwa Machi 14, 2015, kwa sababu ya kufanya mkutano wenye amani wa kidini nyumbani kwake katika eneo la Turkmenabad na akahukumiwa kufungwa na Mahakama ya Eneo la Lebap Mei 19, 2015. Ni kawaida kwa Serikali ya Turkmenistan kuwapa wafungwa msamaha mara tatu kwa mwaka, lakini kila mara Bw. Hemdemov alipuuzwa, ingawa kuna wauaji walioachiliwa katika muda huo. Agosti 15, 2016, Bw. Hemdemov alituma malalamiko kwenye Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu (CCPR), lakini bado hayajashughulikiwa. Mashahidi 11 wa Yehova bado wako gerezani nchini Turkmenistan kwa kukataa kujiunga na jeshi licha ya maamuzi kumi ya CCPR dhidi ya serikali hiyo kwa kuwatesa na kuwafunga vijana Mashahidi ambao wamekataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri.