Hamia kwenye habari

FEBRUARI 15, 2016
TURKMENISTAN

Atimiza Mwaka Mmoja wa Kifungo Kisicho cha Haki Nchini Turkmenistan

Atimiza Mwaka Mmoja wa Kifungo Kisicho cha Haki Nchini Turkmenistan

Kufikia mwezi wa Machi, itakuwa imetimia mwaka mmoja tangu wenye mamlaka wamfunge gerezani Bahram Hemdemov kwa kufanya mkutano wa kidini kwa amani nyumbani kwake jijini Turkmenabad, Turkmenistan. Machi 14, 2015, polisi walivamia nyumba yake, wakamkamata, na wakampiga sana, kisha akahukumiwa kifungo cha miaka minne na kupelekwa kwenye kambi ya kazi ngumu ya Seydi.

Katiba ya Turkmenistan inatetea haki ya “kufuata imani ya dini yoyote ukiwa peke yako au ukishirikiana na wengine” na haki ya “uhuru wa imani na wa kuwaeleza wengine imani hiyo.” Hata hivyo, Bahram bado amefungwa gerezani chini ya hali ngumu kwa sababu tu ya kufuata imani yake. Mashahidi wa Yehova wanawasihi wenye mamlaka wamwachilie huru.