Hamia kwenye habari

JULAI 11, 2019
UGIRIKI

Athens, Ugiriki—Kusanyiko la Kimataifa la 2019 la “Upendo Haushindwi Kamwe”!

Athens, Ugiriki—Kusanyiko la Kimataifa la 2019 la “Upendo Haushindwi Kamwe”!
  • Tarehe: Julai 5-7, 2019

  • Mahali: Uwanja wa Michezo wa Olimpiki jijini Athens, Ugiriki

  • Lugha ya Programu: Kialbania, Kigiriki, Kiingereza, Kiromani (kusini mwa Ugiriki), Kirusi, Lugha ya Ishara ya Ugiriki

  • Idadi ya Wahudhuriaji: 36,873

  • Idadi ya Waliobatizwa: 406

  • Idadi ya Wajumbe Kutoka Mataifa Mbalimbali: 6,000

  • Ofisi za Tawi Zilizoalikwa: Albania, Amerika ya Kati, Armenia, Australasia, Bulgaria, Fiji, Japani, Kyrgyzstan, Makedonia Kaskazini, Marekani, Ulaya ya Kati, Uturuki

  • Mambo Yaliyoonwa: Wakala wa usafiri alisema: “Nimefanya kazi kama wakala wa usafiri maisha yangu yote, na sijawahi kamwe kuona mahali popote ulimwenguni njia bora hivyo ya kupanga na kusimamia wasafiri. Niliwatazama jana, na sikuamini! Mliwapanga watu 2,600 kwa saa chache tu kwa njia bora kuliko wataalamu wengi. Lakini jambo bora zaidi ni jinsi mnavyotabasamu. Kwa kweli, nimefanya kazi hii kwa miaka mingi, na ninaweza kutambua mtu anapotabasamu ‘kikazi’ na wanapotabasamu kutoka moyoni. Nyote mtabasamu kutoka moyoni.”

 

Baadhi ya zaidi ya wajitoleaji 4,000 wakitayarisha uwanja kabla ya kusanyiko

Watoto wakiwakaribisha wajumbe nchini Ugiriki

Mmoja wa ndugu na dada 406 waliobatizwa

Akina dada kwenye sehemu ya Kiromani wakipigwa picha kusanyikoni. Hili lilikuwa kusanyiko la kwanza nchini Ugiriki lililokuwa na lugha ya Kiromani

Wajumbe wakihubiri pamoja na ndugu na dada wenyeji

Wajumbe wakitembelea magofu ya kale ya Ugiriki

Drama ya Biblia iliyoigizwa katika tafrija ya jioni kuhusu huduma ya Mtume Paulo huko Ugiriki

Watumbuizaji wakiwaburudisha wajumbe kwa dansi maarufu ya Syrtaki

Dada akicheza bouzouki, ala ya kitamaduni ya Ugiriki

Wajumbe wakijifunza maneno ya Kigiriki

Ndugu David Splane, mshiriki wa Baraza Linaloongoza, akitoa hotuba ya mwisho siku ya pili ambayo ilitafsiriwa katika Kigiriki

Watumishi wa pekee wa wakati wote wakiwaaga wasikilizaji siku ya mwisho ya kusanyiko