Hamia kwenye habari

JULAI 27, 2018
UGIRIKI

Moto wa Msituni Nchini Ugiriki

Moto wa Msituni Nchini Ugiriki

Moto wa msituni, uliozidishwa na upepo mkali sana, umeharibu mali na kuua watu nje ya jiji la Athens, Ugiriki. Watu 76 hivi wamekufa na wengine 187 wamejeruhiwa katika moto huo, ambao unafikiriwa kuwa moto mbaya zaidi nchini kwa zaidi ya miaka kumi.

Ofisi ya tawi ya Ugiriki imeripoti kwamba hakuna ndugu aliyejeruhiwa au kufa kwa sababu ya janga hili. Hata hivyo, ndugu wote kwenye maeneo yaliyoathiriwa wamelazimika kuhama na sasa wanaishi kwenye nyumba za ndugu katika makutaniko jirani. Pia, nyumba nne za Mashahidi zimeharibiwa kwa kiasi kikubwa na moja imeharibiwa kabisa.

Tunasali kwa ajili ya ndugu zetu walioathiriwa na janga hili na vilevile wale waliochochewa na upendo wa kindugu kuwapokea Mashahidi wenzao. (Yohana 13:34, 35) Tunajua kwamba Yehova ataendelea kuwategemeza ndugu zetu chini ya hali hizo ngumu.