NOVEMBA 4, 2014
UGIRIKI
Habari Kuhusu Kusanyiko la Kimataifa: Mashahidi wa Yehova Wakusanyika Katika Uwanja wa Olympic Nchini Ugiriki
ATHENS, Ugiriki—Mashahidi wa Yehova nchini Ugiriki walifanya Kusanyiko la Kimataifa lenye kichwa “Endeleeni Kuutafuta Kwanza Ufalme wa Mungu!” katika Uwanja wa Olympic Athletic Center huko Athens. Huo ndio uwanja uliotumiwa pia kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya mwaka wa 2004 iliyofanyika Juni 27-29, 2014. Watu 35,863 walikusanyika katika uwanja huo. Wakati wa sehemu fulani za programu hiyo, watu wengine 3,093 waliunganishwa kupitia video nchini Saiprasi na Ubelgiji, kwa hiyo jumla ya wahudhuriaji ilikuwa 38,956.
Wajumbe kutoka Afrika Kusini, Hungaria, Korea, Kroatia, Marekani, Rumania, na Uturuki walihudhuria kusanyiko hilo. Christina Michail, msimamizi wa sehemu kuu ya uwanja wa Olympic, alisema hivi: “Lilikuwa jambo lenye kupendeza sana kuwaona watu wa rangi tofauti na kutoka nchi tofauti, wakiwa wameketi pamoja na wakipiga picha pamoja; nilifurahia sana kuona upendo uliokuwepo kati yao . . . Hilo ni jambo la pekee sana. Si kawaida kuona hivyo katika uwanja huu. Kwa kawaida mashabiki wa michezo ndio huja katika uwanja huu, na tabia yao ni tofauti kabisa; tulifurahia kuona watu tofauti.”
Robert Kern, msemaji wa ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova nchini Ugiriki, alisema hivi: “Tumepokea barua nyingi za shukrani kwa ajili ya programu ya kusanyiko hilo na pia nafasi ya kufurahia ushirika pamoja na ndugu zetu wa mataifa mbalimbali. Ilifurahisha sana kuwa pamoja na waabudu wenzetu kutoka nchi nyingine kwa ajili ya tukio hili la pekee sana.”
Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:
J. R. Brown, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1 718 560 5000
Ugiriki: Babis Andreopoulos, simu +30 210 617 8606