AGOSTI 8, 2019
UHOLANZI
Utrecht, Uholanzi—Kusanyiko la Kimataifa la 2019 la “Upendo Haushindwi Kamwe”!
Tarehe: Agosti 2-4, 2019
Mahali: Jaarbeurs Hallencomplex, Utrecht, Uholanzi
Lugha ya Programu: Kiarabu, Kihispania, Kiholanzi, Kiingereza, Kipapiamento, Kipolandi, Kireno, Kitwi, Lugha ya Alama ya Uholanzi
Idadi ya Wahudhuriaji: 42,335
Idadi ya Waliobatizwa: 212
Idadi ya Wajumbe Kutoka Mataifa Mbalimbali: 6,000
Ofisi za Tawi Zilizoalikwa: Afrika Kusini, Australasia, Brazili, Indonesia, Kanada, Kolombia, Korea, Marekani, Romania, Suriname, Ubelgiji, Ureno
Mambo Yaliyoonwa: Ndugu aliyeajiriwa na kampuni moja ya usafi iliyopewa kandarasi na ukumbi wa Jaarbeurs Hallencomplex alipigiwa simu na meneja mmoja na kuambiwa hivi: “Kuna kikundi hapa ambacho kinafanya kila jambo tulilokubaliana—kwa wakati—wanasafisha jengo na kufanya mipango yao wenyewe ili kudumisha usafi. Inaonekana wataacha jengo likiwa kwenye hali bora kuliko walivyolikuta. Inavutia sana! Sijawahi kuona jambo kama hili. Hata wamesafisha eneo la mkahawa ambalo halitumiki kwa sasa! Kila choo kina watu wawili walio tayari kudumisha usafi; na jambo lolote likitokea, kuna watu walio tayari kusaidia bila kukawia! Sijawahi kamwe kuona jambo kama hili.”
Ndugu na dada wenyeji kwenye uwanja wa ndege wakiwakaribisha wajumbe
Wanabetheli wakiwasalimia wajumbe waliotembelea ofisi ya tawi ya Uholanzi
jumbe akishiriki kampeni ya kugawa mialiko akiwa pamoja na dada mwenyeji
Ndugu na dada wakifurahia programu kwenye ukumbi wa Jaarbeurs Hallencomplex. Maeneo matano yaliunganishwa
Baadhi ya ndugu na dada 212 waliobatizwa
Ndugu na dada wakisikiliza na kuandika mambo makuu wakati wa programu
Wajumbe wa kimataifa wakipeana zawadi
Ndugu Geoffrey Jackson, mshiriki wa Baraza Linaloongoza, akitoa hotuba ya mwisho siku ya Jumapili
Wamishonari na watumishi wengine wa pekee wa wakati wote wakiwapungia mkono wahudhuriaji mwishoni mwa kusanyiko