JUNI 25, 2019
UJERUMANI
Berlin, Ujerumani—Kusanyiko la Kimataifa la 2019 la “Upendo Haushindwi Kamwe”!
Tarehe: Juni 14-16, 2019
Mahali: Uwanja wa Olympiki jijini Berlin, Ujerumani
Lugha ya Programu: Kiingereza, Kijerumani, Kirusi
Idadi ya Wahudhuriaji: 37,115
Idadi ya Waliobatizwa: 255
Idadi wa Wajumbe Kutoka Mataifa Mbalimbali: 5,000
Ofisi za Tawi Zilizoalikwa: Brazili, Uingereza, Kanada, Ekuado, Finland, Ugiriki, Poland, Skandinavia, Slovenia, Marekani
Mambo Yaliyoonwa: Wajumbe walitembelea Jumba la Makumbusho la Pergamon lililopo jijini Berlin kama sehemu ya maeneo waliyotalii karibu na eneo la kusanyiko. Baada ya kuwatazama ndugu zetu waliotembelea makumbusho kwa muda fulani, mlinzi mmoja alisema hivi: “Watu wengi hawana tumaini kwa sababu hawana imani. Ni wazi kabisa kwamba nyinyi mna imani na mna upendo miongoni mwenu wenyewe.” Na mlinzi mwingine alisema hivi: “Kwa wageni kama nyinyi, muda unaenda upesi na ninafurahi kufanya kazi muda wa ziada.”
Ndugu na dada wenyeji wakiwakaribisha wajumbe kwenye uwanja wa ndege
Ndugu na dada wakisalimiana kwenye ua wa eneo la kusanyiko
Wajumbe, baadhi yao wakiwa wamevaa nguo za kitamaduni, wakipiga picha
Ndugu Samuel Herd, mshiriki wa Baraza Linaloongoza, akitoa hotuba ya mwisho siku ya Jumamosi
Wajumbe wakisikiliza programu kwa Kiingereza huku wakiandika mambo makuu kusanyikoni. Wahudhuriaji wawili wakisikiliza programu ikitangazwa kupitia redio kwa kutumia vifaa walivyovaa masikioni
Ndugu na dada wakitazama ubatizo siku ya Jumamosi
Watumishi wa pekee wa wakati wote wakipunga mkono kwenye eneo la kusanyiko mwishoni mwa siku ya Jumapili
Uwanja wa Olympiki jijini Berlin, ambao ulimalizika mwaka wa 1936, picha hii ilipigwa siku ya kwanza ya kusanyiko. Uwanja huu uliwahi kutumika katika kusanyiko la kimataifa la kihistoria lililofanyika Berlin mwaka wa 1990 baada ya Ukuta wa Berlin kuanguka
Wajumbe wakishiriki utumishi wa hadharani mbele ya geti linalofahamika la Brandenburg, jijini Berlin
Wajumbe wakiwa wamekusanyika kwenye Ua wa Colonnade, karibu na Jumba la Makumbusho la Pergamon
Watazamaji wakipiga makofi mwishoni mwa tafrija ya jioni