Hamia kwenye habari

MEI 1, 2013
UJERUMANI

Shahidi wa Yehova Nchini Ujerumani Amepewa Tuzo kwa Sababu ya Huduma Yake Nzuri

Shahidi wa Yehova Nchini Ujerumani Amepewa Tuzo kwa Sababu ya Huduma Yake Nzuri

SELTERS, Ujerumani—Mnamo Februari 22, 2013, Waziri Mkuu wa Bavaria, Horst Seehofer, alimtunuku tuzo Bi. Mathilde Hartl, ambaye ni Shahidi wa Yehova, kwa sababu ya huduma yake nzuri. Hiyo ni tuzo ya heshima inayotolewa na Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani, tuzo ambayo mtu hutunukiwa kwa sababu ya huduma mbalimbali za taifa.

Bi. Hartl, ambaye anaishi Bavaria, alipewa tuzo hiyo ya heshima kwa sababu ya kumhudumia kwa muda mrefu mwanaye Martin, ambaye sasa ana umri wa miaka 26. Alipokuwa mtoto, ilingundulika kuwa Martin ana ugonjwa unaoitwa Duchenne muscular dystrophy (DMD), ugonjwa huo unadhoofisha misuli na hatimaye inaacha kufanya kazi hatua kwa hatua. Kwa sababu ya hali hiyo, Bi. Hartl huwa anamhudumia mwanaye karibu usiku kucha, huduma hiyo inatia ndani kuchunguza kwa ukawaida mashine inayomsaidia kupumua, na kuondoa umajimaji ulio kwenye mrija wa kupitishia hewa ili kuzuia maambukizi au nimonia. Mwanaye mwingine, Max, alikuwa na ugonjwa kama huo wa DMD, lakini zaidi ya ugonjwa huo, pia yeye alikuwa na ulemavu wa akili. Kwa sababu ya upendo wake, Bi. Hartl aliwahudumia Martin na Max kwa miaka mingi. Inasikitisha kwamba, Max alikufa mwaka 2008, akiwa na umri wa miaka 19.

Alipoulizwa kwamba anapata wapi nguvu za kuhudumia kwa njia bora kadiri hiyo, Bi. Hartl alijibu hivi: “Kutoka kwenye dini yangu. Nikiwa Shahidi wa Yehova, ninauheshimu sana uhai. Kwa hiyo, ninafanya yote ninayoweza ili mwanangu awe na furaha licha ya ugonjwa wake.”

Waziri Mkuu Seehofer alimsifu Bi. Hartl na wengine waliopewa tuzo pamoja naye kwa kusema: “Ninyi nyote mmefanya kuwe na nafuu kidogo katika ulimwengu huu.”

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

J. R. Brown, Ofisi ya Habari za Umma, simu. +1 718 560 5000

Ujerumani: Wolfram Slupina, simu. +49 6483 41 3110