SEPTEMBA 27, 2022 | HABARI ZILIONGEZWA: MACHI 22, 2024
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE
HABARI ZA KARIBUNI—HUKUMU YAPINDULIWA | Yehova Awasaidia Kushinda Hisia za Kuvunjika Moyo
Machi 21, 2024, Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Krimea ilipindua hukumu dhidi ya Ndugu Taras Kuzo na mke wake, Dada Darya Kuzo, pamoja na Ndugu Sergey Lyulin na Ndugu Petr Zhiltsov. Waliachiliwa mara moja kutoka kizuizini. Kesi yao sasa itarudishwa kwenye Mahakama ya Jiji la Yalta katika Jamhuri ya Crimea ili isikilizwe upya.
Februari 27, 2023, Mahakama ya Jiji la Yalta katika Jamhuri ya Crimea iliwahukumu Ndugu Taras Kuzo na mke wake, Dada Darya Kuzo, pamoja na Ndugu Sergey Lyulin na Ndugu Petr Zhiltsov. Darya alipewa kifungo cha nje cha miaka mitatu. Hahitaji kwenda gerezani wakati huu. Taras alihukumiwa kifungo cha miaka sita na nusu gerezani. Sergey na Petr walihukumiwa kifungo cha miaka sita na mwezi mmoja, kila mmoja. Ndugu wote watatu walipelekwa gerezani moja kwa moja kutoka mahakamani.
Mfuatano wa Matukio
Machi 4, 2021
Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Taras, na alishtakiwa kwa kuchangia pesa kwa ajili ya shirika lenye msimamo mkali
Machi 11, 2021
Nyumba tisa za Mashahidi wa Yehova zilivamiwa kutia ndani nyumba ya Kuzo na ya Sergey. Taras aliwekwa kizuizuni
Machi 12, 2021
Taras aliachiliwa na kuwekwa kwenye kifungo cha nyumbani, ingawa hakuruhusiwa kuishi na familia yake
Julai 29, 2021
Kesi za uhalifu zilifunguliwa dhidi ya Darya, Petr, na Sergey. Petr aliwekwa kizuizini
Julai 30, 2021
Kesi hizo za uhalifu ziliunganishwa na kuwa kesi moja. Petr aliachiliwa na kuwekwa katika kifungo cha nyumbani
Agosti 10, 2021
Sergey alikamatwa na kusafirishwa hadi eneo lingine lililokuwa umbali wa kilometa 800, na huko akawekwa mahabusu. Safari hiyo ilichukua saa 16, na katika kipindi hicho chote mikono yake ilikuwa imefungwa juu kwenye bomba la chuma na miguu yake ilikuwa imefungwa kwenye kiti alichokalia.
Machi 1, 2022
Sergey aliachiliwa kutoka mahabusu na akawekwa katika kifungo cha nyumbani
Aprili 4, 2022
Kesi ya uhalifu ilianza
Julai 11, 2022
Petr, Sergey, na Taras waliachiliwa kutoka kwenye kifungo cha nyumbani na wakawekewa vizuizi vya kusafiri
Maelezo Mafupi Kuwahusu
Ndugu na dada waaminifu wanapokuwa gerezani, kizuizini, au katika kifungo cha nyumbani, huenda wakahisi wamebanwa “kupita kiasi cha kushindwa kusonga,” lakini Yehova hatawaacha kamwe wale wanaoteswa kwa ajili ya jina lake.—2 Wakorintho 4:8, 9.