JANUARI 23, 2024 | HABARI ZIMEONGEZWA: APRILI 18, 2024
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE
HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU AHUKUMIWA | “Mambo Yote Yanawezekana kwa Mtu Mwenye Imani”
Aprili 16, 2024 Mahakama ya Wilaya ya Nakhimovskiy iliyo katika mji wa Sevastopol ilimhukumu Ndugu Maksim Zinchenko kifungo cha miaka miwili na kazi ngumu. Atahitaji kukaa gerezani na kufanya kazi alizopangiwa kufanya katika jamii.
Maelezo Mafupi Kumhusu
Tuna uhakika kwamba Yehova atabariki ujasiri na uvumilivu wa Maksim na pia wengine wote wanaoendelea kufanya mapenzi Yake.—Waebrania 10:35, 36.
Mfuatano wa Matukio
Mei 17, 2023
Alishtakiwa kwa madai ya kushiriki utendaji wa shirika lenye msimamo mkali
Mei 22, 2023
Nyumba yake ilifanyiwa msako. Maksim na Karina wakahojiwa. Maksim aliwekwa kizuizini
Mei 24, 2023
Maksim alitolewa kizuizini na kuwekwa kwenye kifungo cha nyumbani
Julai 12, 2023
Kesi ya uhalifu ilianza