Hamia kwenye habari

Kushoto: Ndugu Yuriy Gerashchenko na mke wake, Irina. Kulia: Ndugu Sergey Parfenovich na mke wake, Marina

JANUARI 9, 2024 | HABARI ZIMEONGEZWA: OKTOBA 7, 2024
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU WAMEFUNGWA | Kuazimia Kushikamana na Yehova

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU WAMEFUNGWA | Kuazimia Kushikamana na Yehova

Oktoba 3, 2024, Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Crimea ilibadili hukumu iliyokuwa imetolewa kwa Ndugu Yuriy Gerashchenko na Ndugu Sergey Parfenovich. Awali, walikuwa wamehukumiwa kifungo cha nje cha miaka sita lakini sasa wamehukumiwa miaka sita gerezani. Walipelekwa gerezani moja kwa moja baada ya kutoka mahakamani.

Julai 1, 2024, Mahakama ya Wilaya ya Krasnogvardeyskiy iliyo katika Jamhuri ya Crimea iliwahukumu Ndugu Yuriy Gerashchenko na Sergey Parfenovich kifungo cha nje cha miaka sita na hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tunajua kwamba Yehova atawategemeza Yuriy na Sergey, na pia wengine wote wanaodumisha utimilifu wao kadiri anavyoendelea ‘kuwaficha katika kivuli cha mabawa yake.’​—Zaburi 17:7, 8.

Mfuatano wa Matukio

  1. Septemba 19, 2022

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Sergey

  2. Septemba 28, 2022

    Nyumba ya Sergey ilikuwa miongoni mwa nyumba nane ambazo zilifanyiwa msako na maofisa wa FSB, naye aliwekwa kizuizini kwa muda

  3. Septemba 30, 2022

    Sergey alipelekwa mahabusu

  4. Novemba 15, 2022

    Sergey aliachiliwa kutoka mahabusu na kuwekwa kwenye kifungo cha nyumbani

  5. Machi 22, 2023

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Yuriy. Alikamatwa, akahojiwa, na kuwekwa mahabusu

  6. Machi 24, 2023

    Yuriy aliachiliwa na kuwekwa kwenye kifungo cha nyumbani

  7. Julai 12, 2023

    Sergey na Yuriy waliachiliwa kutoka kwenye kifungo cha nyumbani na kuwekewa vizuizi vya kusafiri

  8. Julai 28, 2023

    Kesi ya uhalifu ilianza. Mwendesha-mashtaka aliwashtaki Sergey na Yuriy kwa sababu ya kuendelea “kujihusisha katika utendaji wa kihalifu na kuwatisha mashahidi.” Licha ya kwamba hakuwa na ushahidi wowote, hakimu aliamua kuwaweka kwenye kifungo cha nyumbani kwa mara nyingine tena