Hamia kwenye habari

Ndugu Artem Gerasimov

FEBRUARI 27, 2020
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE

Hivi Karibuni Mahakama ya Crimea Itatangaza Hukumu ya Kesi ya Ndugu Artem Gerasimov

Hivi Karibuni Mahakama ya Crimea Itatangaza Hukumu ya Kesi ya Ndugu Artem Gerasimov

Machi 3,2020, Mahakama ya Jiji la Yalta la Jamhuri ya Crimea inatarajiwa kutangaza hukumu ya kesi ya Ndugu Artem Gerasimov. Mwendesha mashtaka ameomba Ndugu Gerasimov afungwe miaka sita na nusu gerezani kwa sababu ya imani yake.

March 20, 2019, Ndugu  Gerasimov alikamatwa na kuhojiwa baada ya Maofisa wa Federal Security Service (FSB) kuvamia nyumba nane za Mashahidi wa Yehova wanaoishi katika majiji ya Alupka na Yalta nchini Crimea. Msako ulipokuwa ukiendelea, maofisa hao walichukua kompyuta na vifaa vingine vya kielektroni pamoja na Biblia. Kisha wachunguzi wa FSB wakamshtaki Artem Gerasimov kwa kosa la kupanga shughuli zenye msimamo mkali, kwa sababu tu alikuwa akikukutana na wengine ili kuzungumzia Biblia.

Tuna uhakika kabisa kwamba Yehova atawasaidia ndugu na dada zetu kubaki ‘jasiri na wenye nguvu’ kadiri wanavyoendelea kuvumilia mashambulizi dhidi ya imani yao.—Zaburi 138:3.