NOVEMBA 11, 2022
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE
Mradi wa Makao Makuu wa Ramapo
Kamati ya Mipango ya Mji Yakubali Badiliko la Matumizi ya Ardhi na Hivyo Kufungua Njia ya Kupata Idhini ya Ramani
Novemba 9, 2022, Kamati ya Mji la Ramapo ilikubali badiliko la matumizi ya ardhi katika eneo la mradi wa ujenzi wa Ramapo. Hilo litawezesha Halmashauri ya Mradi wa Ujenzi wa Ramapo (CPC) kuanza kufuatilia kibali cha pekee na pia idhini ya ramani ili mradi wa ujenzi uanze. a
Zaidi ya hilo, wakandarasi wamepanua na kurekebisha barabara inayoingia kwenye eneo la mradi wa Ramapo. Vilevile, wajitoleaji wa ujenzi wamemaliza kurekebisha daraja la mawe lililo kwenye barabara hiyo, karibu tu na mwiingilio wa eneo la ujenzi. Kazi hiyo ya kurekebisha daraja ilitia ndani kulipanua na kuliimarisha ili ambulansi na magari ya zima-moto yaweze kupita, bila kusahau usafirishaji wa vifaa vya ujenzi. Katika kipindi cha mwanzo cha ujenzi, magari yote yatatumia daraja hilo.
Ndugu Matthew Mordecki, ambaye anatumikia kwenye Halmashauri ya Mradi wa Ujenzi anasema: “Badiliko katika matumizi ya ardhi linatuwezesha kufuatilia kibali cha pekee na idhini ya ramani kwa wakati uleule. Tukipata kibali hicho tunaweza kuanza kutayarisha uwanja mapema mwezi wa Desemba 2022.”
Tunasali kwamba Yehova aendelee ‘kuwapa mafanikio’ ndugu na dada wanaofanya kazi moja kwa moja katika mradi huu wa ujenzi.—Nehemia 1:11.
a Kabla ya badiliko hili la matumizi ya ardhi, eneo hilo la ujenzi lilikuwa limetengwa kwa ajili makazi ya watu wenye umri mkubwa au wenye mahitaji ya pekee.