JANUARI 9, 2023
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE
Mradi wa Makao Makuu ya Ramapo
Kamati ya Mji wa Ramapo Yatoa Kibali cha Pekee
Desemba 28, 2022, Kamati ya Mji wa Ramapo ilikubali kutoa kibali cha pekee kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Ramapo. a Kibali hiki cha pekee kinatuwezesha kujenga ofisi, studio, na pia makao katika eneo hilo. Isitoshe, kibali hicho kinatuwezesha kung’oa miti na kutayarisha eneo kwa ajili ya ujenzi huku tukisubiria idhini ya ramani kutoka kwa Kamati ya Mipango ya Mji. Idhini hiyo inatarajiwa kupatikana mwishoni mwa mwaka wa 2023. Kwa hiyo, kibali hicho cha pekee kitasaidia mradi kusonga kwa muda uliopangwa.
Ndugu David Soto, anayetumikia kwenye Halmashauri ya Mradi wa Ujenzi anasema: “Tumefurahi sana kupata kibali hiki. Ingawa bado kuna hatua nyingine ambazo zitahitaji kuchukuliwa kabla ya ujenzi wenyewe kuanza, tuna uhakika Yehova ataendelea kubariki jitihada zetu.”
Mfuatano wa Matukio wa Ujenzi wa Mradi wa Ramapo
Oktoba 5, 2019
Juni 26, 2020
Ombi la ujenzi lawasilishwa kwenye Kamati ya Mji wa Ramapo
Julai 8, 2020
Mkutano wa kwanza wafanywa pamoja na Kamati ya Mji wa Ramapo
Machi 31, 2021
Hati ya kwanza inayofafanua jinsi mazingira yatakavyoathiriwa na ujenzi yawasilishwa
Machi 8, 2022
Kamati ya Mipango ya Mji wa Tuxedo yatoa kibali cha kurekebisha na kupanua barabara ya kuingia kwenye mradi wa Ramapo
Machi 12, 2022
Hati ya mwisho inayofafanua jinsi mazingira yatakavyoathiriwa na ujenzi yakubaliwa
Novemba 9, 2022
Kamati ya Mji wa Ramapo yakubali badiliko la matumizi ya ardhi na hivyo kuturuhusu kujenga ofisi na makao pia
Desemba 28, 2022
Kamati ya Mji wa Ramapo yakubali kutoa kibali cha pekee kinachotuwezesha kujenga majengo yenye matumizi mbalimbali na pia kung’oa miti na kutayarisha uwanja kwa ajili ya ujenzi
Kinachosubiriwa
Idhini ya ramani kamili ya ujenzi
a Novemba 9, 2022, Kamati ya Mji wa Ramapo ilikubali badiliko la matumizi ya ardhi ya eneo la ujenzi. Hilo lilitufungulia njia ya kuwasilisha kwa wakati mmoja maombi kwa ajili ya idhini ya ramani na pia kibali cha pekee.