Hamia kwenye habari

Ndugu Sergey Filatov

MACHI 2, 2020
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE

Kesi ya Kwanza Inayomhusu Shahidi wa Yehova Huko Crimea Yasubiri Uamuzi

Kesi ya Kwanza Inayomhusu Shahidi wa Yehova Huko Crimea Yasubiri Uamuzi

Machi 5, 2020, Mahakama ya Wilaya ya Dzhankoysky huko Jamhuri ya Crimea, yatarajiwa kutangaza uamuzi wake katika kesi inayomhusu Ndugu Sergey Filatov. Mwendesha-mashtaka ameomba mahakama imhukumu kifungo cha miaka saba katika gereza lenye ulinzi mkali. Ndugu Filatov ndiye Shahidi wa kwanza huko Crimea kuhukumiwa chini ya Sheria ya Uhalifu ya Urusi.

Kama ilivyoripotiwa awali, Ndugu Filatov alikamatwa katika moja kati ya misako mikubwa na uvamizi dhidi ya ndugu zetu katika miaka ya hivi karibuni. Oktoba 10, 2017, marafiki pamoja watu wengine walikusanyika katika nyumba ya Ndugu Filatov ili kuzungumzia Biblia na kuimba nyimbo za Ufalme. Maofisa wa Usalama wa Taifa nchini Urusi (FSB), walirekodi mkutano huo kwa siri. Baada ya mwaka mmoja, usiku wa Novemba 15, 2018, maofisa karibu 200 walivamia nyumba nane za Mashahidi wa Yehova katika eneo hilo. Zaidi ya maofisa wa polisi 35, walifanya msako katika nyumba ya Ndugu Filatov, na wengi wao walikuwa wanajeshi wa vikosi maalum waliokuwa na silaha. Ndugu Filatov alihojiwa kisha akaachiliwa.

Ndugu Sergey Filatov na mke wake, Natalya, wana watoto wanne, na wawili kati yao bado ni wadogo sana. Ndugu Filatov anapoendelea kusubiri uamuzi wa mahakama, tunasali kwamba yeye na familia yake waendelee kumfanya Yehova kuwa kimbilio lao, wakiwa na uhakika kwamba atawasaidia katika hali hii ngumu.—Zaburi 46:1.