Hamia kwenye habari

Picha ya satelaiti ya Kimbunga Beryl kikiwa juu ya Rasi ya Yucatán iliyoko Mexico, Julai 5, 2024

JULAI 12, 2024
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE

Kimbunga Beryl Kimewaathiri Mamilioni ya Watu

Kimbunga Beryl Kimewaathiri Mamilioni ya Watu

Juni 30, 2024, Kimbunga Beryl kilipita upande wa kusini wa kisiwa cha Martinique, kilichoko West Indies. Siku iliyofuata, kimbunga hicho kiliongezeka ukubwa na kupiga Visiwa vya Windward, vinavyotia ndani Barbados, Grenada, na Saint Vincent na Grenadines. Siku iliyofuata kimbunga hicho kiliongezeka tena ukubwa na kuipiga Venezuela. Kisha kimbunga hicho kikapita karibu sana na pwani ya Jamaika. Julai 5, kimbunga hicho chenye nguvu kilipiga Rasi ya Yucatán iliyoko Mexico kabla ya kufika kusini mwa Marekani.

Kila mahali ambapo kimbunga hicho kilipita, kilisababisha mvua kubwa na upepo wenye nguvu unaofikia mwendo wa kilomita 270 kwa saa, na hivyo kuharibu nyumba, biashara, na miundo mbinu. Mamilioni ya watu wanaoishi katika maeneo yaliyoathiriwa bado hawana umeme, maji, na huduma nyingine za msingi. Ripoti zinaonyesha kwamba zaidi ya watu 30 wamekufa.

Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata

Martinique (West Indies)

  • Hakuna ndugu au dada aliyekufa au kujeruhiwa

  • Wahubiri 6 walilazimika kuhama makao yao

  • Nyumba 1 iliharibiwa kabisa

  • Nyumba 1 ilipata uharibifu mkubwa

  • Nyumba 1 ilipata uharibifu mdogo

  • Hakuna Jumba la Ufalme ambalo liliharibiwa

Jumba la Ufalme lililopata uharibifu kwenye Visiwa vya Windward

Visiwa vya Windward

  • Hakuna ndugu au dada aliyekufa

  • Wahubiri 7 walipata majeraha

  • Wahubiri 67 walilazimika kuhama makao yao

  • Nyumba 39 zilipata uharibifu mkubwa

  • Nyumba 31 zilipata uharibifu mdogo

  • Jumba 1 la Ufalme liliharibiwa kabisa

  • Jumba 1 la Ufalme lilipata uharibifu mkubwa

  • Majumba 4 ya Ufalme yalipata uharibifu mdogo

Venezuela

  • Hakuna ndugu au dada aliyekufa au kujeruhiwa

  • Wahubiri 30 walilazimika kuhama makao yao

  • Nyumba 12 zilipata uharibifu mkubwa

  • Nyumba 9 zilipata uharibifu mdogo

  • Jumba 1 la Ufalme lilipata uharibifu mkubwa

Jamaika

  • Hakuna ndugu au dada aliyekufa au kujeruhiwa

  • Wahubiri 18 walilazimika kuhama makao yao

  • Nyumba 24 zilipata uharibifu mkubwa

  • Nyumba 75 zilipata uharibifu mdogo

  • Majumba 19 ya Ufalme yalipata uharibifu mdogo

Mexico

  • Hakuna ndugu au dada aliyekufa au kujeruhiwa

  • Wahubiri 320 walilazimika kuhama makao yao lakini sasa wamerudi nyumbani

  • Nyumba 11 zilipata uharibifu mdogo

  • Hakuna Jumba la Ufalme ambalo liliharibiwa

Marekani

  • Hakuna ndugu au dada aliyekufa

  • Wahubiri 6 walipata majeraha

  • Wahubiri 242 walilazimika kuhama makao yao

  • Nyumba 4 ziliharibiwa kabisa

  • Nyumba 33 zilipata uharibifu mkubwa

  • Nyumba 471 zilipata uharibifu mdogo

  • Hakuna Jumba la Ufalme ambalo liliharibiwa

Jitihada za Kutoa Msaada

Waangalizi wa mzunguko na wazee katika maeneo hayo mbalimbali wanatoa msaada wa kiroho na wa kimwili kwa wote walioathiriwa. Isitoshe, Halmashauri sita za Kutoa Msaada zimewekwa rasmi ili kusimamia jitihada za kutoa msaada.

Tunasali kwamba Yehova aendelee kuwafariji wote wanaomtumaini katika kipindi hiki kigumu.​—2 Wakorintho 1:3, 4.