NOVEMBA 20, 2020
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE
Kimbunga Eta Chashambulia Amerika ya Kati, Visiwa vya Cayman, Bahamas, Jamaika, Mexico, na Marekani
Mahali
Amerika ya Kati, Visiwa vya Cayman, Bahamas, Jamaika, Mexico, na kusini-mashariki mwa Marekani
Janga
Novemba 3, 2020, kimbunga Eta kilishambulia mji wa Puerto Cabezas, Nikaragua na sehemu nyingine za Amerika ya Kati, na kusababisha uharibifu mkubwa sana
Inasikitisha kwamba kijana mjukuu mwenye umri wa miaka tisa wa wenzi Mashahidi wanaoishi Tabasco, Mexico, alikufa baada ya kuchukuliwa na mafuriko
Mwishowe kimbunga Eta kilipungua na kuwa dhoruba ya kitropiki iliyoathiri Kisiwa cha Grand Cayman, Bahamas, na Jamaika. Dhoruba hiyo ilipiga pia Ghuba ya Mexico na kuathiri Marekani
Athari ambazo ndugu na dada zetu wamepata
Kosta Rika
Wahubiri 108 wamelazimika kuhama makazi yao
Wahubiri 7 walipoteza mali zao zote
Guatemala
Awali wahubiri 163 walilazimika kuhama makazi yao; kufikia sasa wahubiri 85 wamerudi katika makazi yao
Familia 3 zilipoteza mali zao zote
Kwa kuongezea, familia 1 iliyo na wahubiri 3, ilinaswa katika ghorofa ya pili ya nyumba yao mpaka walipookolewa
Honduras
Mwanzoni wahubiri 1,984 walilazimika kuhama makazi yao; wahubiri 376 hivi wamerudi katika makazi yao
Jamaika
Wahubiri 4 walilazimika kuhama makazi yao
Mexico
Katika majimbo ya Chiapas na Tabasco, wahubiri 1,618 walihamishwa kutoka katika makazi yao; 112 wamerudi katika makazi yao
Nikaragua
Wahubiri 238 walilazimika kuhama makazi yao; 232 wamerudi katika makazi yao
● Panama
Wahubiri 27 walilazimika kuhama makazi yao; 6 wamerudi katika makazi yao
Marekani
Wahubiri 48 walilazimika kuhama makazi yao; 27 wamerudi katika makazi yao
Uharibifu wa mali
Bahamas
Nyumba 1 iliharibiwa
Kosta Rika
Nyumba 3 ziliharibiwa
Nyumba 6 ziliharibiwa
Guatemala
Nyumba 2 ziliharibiwa na maporomoko ya ardhi
Honduras
Majumba ya Ufalme 7 yaliharibiwa kidogo
Nikaragua
Nyumba 73 ziliharibiwa
Kisiwa cha Grand Cayman
Nyumba 4 ziliharibiwa
Jumba la Ufalme 1 liliharibiwa kidogo
Jamaika
Nyumba 50 ziliharibiwa
Jumba la Ufalme 1 liliharibiwa
Marekani
Nyumba 141 ziliharibiwa
Majumba ya Ufalme 9 yaliharibiwa kidogo
Jitihada za kutoa msaada
Ofisi ya tawi ya Amerika ya Kati imeweka rasmi Halmashauri tatu za Kutoa Misaada (DRC), mbili Mexico na moja Honduras, ili kuratibu utoaji misaada. Katika nchi nyingine zilizoathiriwa, DRC zilizopewa kazi ya kutoa misaada kwa sababu ya maafa yaliyoletwa na ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19), zinasaidia pia katika kutoa msaada kwa walioathiriwa na kimbunga
Katika eneo la ofisi ya tawi ya Marekani, makutaniko pamoja na DRC zilizowekwa ili kutoa msaada kwa sababu ya maafa yaliyoletwa na COVID-19 katika maeneo hayo, wanatoa msaada pia
Waangalizi wa mzunguko katika maeneo hayo wanaendelea kufariji familia zilizoathiriwa kwa kutumia maandiko
Ndugu na dada wanaoishi katika maeneo salama wametoa makazi na chakula kwa wote waliolazimika kuhama nyumba zao
Kazi yote ya kutoa misaada inafuata miongozo ya kujihadhari na ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19)
Ijapokuwa dhoruba hiyo imeleta uharibifu mkubwa, tunatiwa moyo kuona jinsi ndugu zetu wanavyosaidiana. Tunajua kwamba Mungu wetu, Yehova ‘atakuwa kimbilio salama katika nyakati za taabu.’—Zaburi 9:9.