SEPTEMBA 26, 2022
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE
Kimbunga Fiona Kimesababisha Uharibifu Mkubwa Katika Eneo la Karibea
Septemba 18, 2022, Kimbunga Fiona kilipita nchini Puerto Riko na visiwa vilivyo karibu. Kimbunga hicho kiliambatana na upepo mkali uliovuma umbali wa kilomita 160 kwa saa pamoja na mvua kubwa. Dhoruba hiyo iliharibu barabara na madaraja na kuwaacha maelfu bila umeme. Kuharibiwa kwa barabara na madaraja, kunafanya iwe vigumu kwa serikali kupeleka chakula na dawa kwa walioathiriwa.
Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata
Puerto Riko, Saint Kitts na Nevis, Turks na Caicos
Hakuna ndugu au dada ambaye amekufa
Wahubiri 4 wamepata majeraha madogo
Wahubiri 75 wamelazimika kuhama makazi yao
Nyumba 140 zimepata uharibifu mdogo
Nyumba 18 zimepata uharibifu mkubwa
Nyumba 1 imeharibiwa kabisa
Jamhuri ya Dominika
Hakuna ndugu au dada ambaye amekufa
Wahubiri 58 wamelazimka kuhama makazi yao
Nyumba 57 zimepata uharibifu mdogo
Nyumba 26 zimepata uharibifu mkubwa
Nyumba 2 zimeharibiwa kabisa
Majumba 2 ya Ufalme yamepata uharibifu mdogo
Majumba 2 ya Ufalme yamepata uharibifu mkubwa
Guadeloupe na Martinique
Hakuna ndugu au dada ambaye amekufa
Wahubiri 16 wamelazimika kuhama makazi yao
Nyumba 43 zimepata uharibifu mdogo
Nyumba 2 zimepata uharibifu mkubwa
Majumba 13 ya Ufalme yamepata uharibifu mdogo
Jitihada za Kutoa Msaada
Waangalizi wa mzunguko na wazee wa makutaniko wanafanya ziara za uchungaji kwa familia zilizoathiriwa na kuandaa msaada unaohitajika
Mipango imeanza kufanywa ili kupeleka misaada kwa familia zilizoathiriwa na kurekebisha nyumba zilizoharibiwa
Jitihada zote za kutoa msaada zinafanywa kupatana na miongozo ya kujilinda dhidi ya ugonjwa wa COVID-19
Tunajua kwamba ndugu na dada zetu walioathiriwa na kimbunga hicho watapata faraja kupitia matendo ya upendo kutoka kwa ndugu zetu.—Matendo 11:29.