Hamia kwenye habari

Kimbunga Ian kilisababisha uharibifu mkubwa na kuwaacha mamilioni ya watu nchini Kuba na Marekani bila umeme

OKTOBA 4, 2022
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE

Kimbunga Ian Chasababisha Uharibifu Mkubwa

Kimbunga Ian Chasababisha Uharibifu Mkubwa

Septemba 27, 2022, Kimbunga Ian kilisababisha uharibifu mkubwa nchini Kuba na siku iliyofuata kimbunga hicho chenye nguvu kilifika upande wa kusini-magharibi mwa Florida. Kimbunga Ian kilikuwa mojawapo ya vimbunga vyenye nguvu zaidi kutokea Marekani na kilikuwa na upepo wenye kasi ya kilometa 240 kwa saa. Kimbunga hicho kiliharibu nyumba nyingi, kikasababisha umeme kukatika, kikaharibu barabara na madaraja, kikaleta mafuriko katika maeneo ambayo kilipitia na kikaenda hadi kwenye Bahari ya Atlantiki. Baada ya hapo kikafika katika jimbo la South Carolina.

Kwa sababu ya kimbunga hicho hatari wahubiri 12,000 katika jimbo la Florida walilazimika kuhama makazi yao.

Waangalizi wa mzunguko wanashirikiana na wawakilishi wa Idara ya Usanifu-Majengo na Ujenzi ili kuwasaidia wazee kushughulikia mahitaji ya msingi ya ndugu na dada walioathiriwa.

Athari ambazo ndugu na dada zetu wamepata

Kuba

  • Kwa kusikitisha, ndugu 1 alikufa

  • Ndugu 2 walipata majeraha madogo

  • Nyumba 300 zilipata uharibifu mdogo

  • Nyumba 491 zilipata uharibu mkubwa

  • Nyumba 63 ziliharibiwa kabisa

  • Sehemu 40 za kukutana zilipata uharibifu mkubwa

  • Sehemu 1 ya kusanyiko ilipata uharibifu mdogo

  • Sehemu 3 za kusanyiko zilipata uharibifu mkubwa

Florida

  • Hakuna ndugu au dada aliyeuawa katika kimbunga hicho

  • Wahubiri 2 walipata majeraha madogo

  • Wahubiri 5,874 wamelazimika kuhama makao yao

  • Nyumba 1,559 zilipata uharibifu mdogo

  • Nyumba 367 zilipata uharibifu mkubwa

  • Nyumba 47 ziliharibiwa kabisa

  • Kufikia sasa nyumba 329 zimerekebishwa kwa kiasi fulani

  • Kufikia sasa nyumba 71 zimefanyiwa ukarabati mkubwa

  • Majengo 38 ya kitheokrasi yalipata uharibifu mdogo

  • Jumba 1 la Ufalme lilipata uharibifu mkubwa

  • Jumba 1 la Kusanyiko lilipata uharibifu mkubwa

South Carolina

  • Hakuna ndugu au dada aliyeuawa katika kimbunga hicho

  • Wahubiri 35 wamelazimika kuhama makao yao

  • Nyumba 13 zilipata uharibifu mdogo

Jitihada za Kutoa Msaada

  • Waangalizi wa mzunguko pamoja na wazee wa makutaniko wanafanya ziara za uchungaji na kuwapa wahubiri walioathiriwa na msiba huo msaada unaohitajika

  • Ili kuwasaidia akina ndugu na dada, vituo 14 vya muda vya kutoa msaada vimewekwa katika barabara za jimbo la Florida ambazo hutumiwa na watu wanaokimbilia maeneo salama zaidi

  • Halmashauri za Kutoa Msaada zilianzishwa katika Florida na Kuba ili kusimamia jitihada za kutoa msaada

  • Jitihada zote za kutoa msaada zinafanywa kupatana na miongozo ya kujilinda na COVID-19

Ndugu zetu huwasaidia waabudu wenzao wanapokabili majanga, hivyo basi ukweli wa maneno haya ya mtunga zaburi unaonekana wazi: “Mtu anayemtumaini Yehova amezungukwa na upendo Wake mshikamanifu.”​—Zaburi 32:10.