SEPTEMBA 4, 2023
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE
Kuimarisha Imani Ili Kushinda Woga
Mahakama ya Wilaya ya Gagarinskiy iliyo Sevastopol, Crimea, itatangaza hivi karibuni uamuzi wake katika kesi inayowahusu Ndugu Viktor Kudinov na Ndugu Sergey Zhigalov. Mwendesha-mashtaka bado hajatoa ombi la hukumu anayopendekeza.
Maelezo Mafupi Kuwahusu
Yehova ni Mungu “anayefurahia amani ya [watumishi] wake.” Kwa hiyo, tuna uhakika kwamba ataendelea kuwabariki Viktor na Sergey kwa sababu wanaonyesha subira na uvumilivu.—Zaburi 35:27.
Mfuatano wa Matukio
Agosti 24, 2022
Kesi ya uhalifu yafunguliwa. Nyumba zao zafanyiwa msako. Wanakamatwa na kuwekwa kizuizini
Agosti 26, 2022
Wanaachiliwa kutoka kizuizini na kuwekwa katika kifungo cha nyumbani
Oktoba 17, 2022
Wanaachiliwa kutoka kwenye kifungo cha nyumbani na kuwekewa vizuizi vingine
Aprili 13, 2023
Kesi ya uhalifu yaanza