Hamia kwenye habari

JUNI 4, 2020
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE

Mahakama Kuu ya Crimea Yamhukumu Ndugu Artem Gerasimov Kifungo cha Miaka Sita Gerezani

Mahakama Kuu ya Crimea Yamhukumu Ndugu Artem Gerasimov Kifungo cha Miaka Sita Gerezani

Juni 4,2020, Mahakama Kuu ya Crimea ilimhukumu Ndugu Artem Gerasimov kifungo cha miaka sita gerezani kwa sababu ya kuendelea kufanya ibada akiwa Mkristo. Alikuwa amekata rufaa baada ya kuhukumiwa na Mahakama ya jiji la Yalta, ambako alitozwa faini ya rubo 400,000 (au dola 6,000 hivi za Marekani). Hukumu hiyo ilitekelezwa mara moja na Ndugu Gerasimov akafungwa gerezani. Atakata rufaa uamuzi huo.