Hamia kwenye habari

Picha iliyopigwa kutoka juu ya eneo la Ramapo. Eneo lisilo na miti linaonyesha ukubwa wa eneo la ujenzi. Picha ndogo: Mkataji wa miti akitumia msumeno

JUNI 6, 2023
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE

Mradi wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Ramapo

Matayarisho Kwenye Eneo la Ujenzi la Ramapo Yanaendelea

Matayarisho Kwenye Eneo la Ujenzi la Ramapo Yanaendelea

Juni 1, 2023, Idara ya Kuhifadhi Mazingira ya Jimbo la New York iliidhinisha ombi la kuondoa miti iliyokatwa katika eneo la ujenzi la Ramapo. Kazi ya kukata miti ilikamilishwa Machi 18, majuma mawili hivi kabla ya muda ulioruhusiwa wa kukata miti.

Ndugu Robert McRedmond, anayetumikia akiwa mratibu wa Halmashauri ya Mradi wa Ujenzi (CPC) katika mradi wa Ramapo, alisema hivi: “Tunatambua kwamba wakati wa miradi mikubwa kama huu, kila idhini na kibali kinachotolewa kinatuleta karibu sana kuanza ujenzi wenyewe. Tumemwona Yehova akiondoa vikwazo, na tunatarajia kuona jinsi atakavyotusaidia kushinda vikwazo vyovyote vitakavyojitokeza wakati ujao.”​—Isaya 57:14.

Halmashauri ya Mradi wa Ujenzi inaendelea kushirikiana na wenye mamlaka ili kupata vibali vyote.