DESEMBA 31, 2021
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE
Mnara wa Mlinzi Na. 2 Toleo la Watu Wote Limesambazwa Katika Zaidi ya Lugha 300 Wakati wa Kampeni ya Novemba
Lugha Saba Mpya Zatolewa!
Novemba 2021, Mashahidi wa Yehova ulimwenguni pote walisambaza toleo la watu wote la Mnara wa Mlinzi Na. 2 2021 katika zaidi ya lugha 300. Kwa saba kati ya lugha hizo, toleo hilo Na. 2 2021 lilikuwa toleo la kwanza la Mnara wa Mlinzi kutafsiriwa katika lugha yao. Lugha hizo zinatia ndani: Kifaroe, Kikrioli cha Saint Lucian, Kiluxembourg, Kimanipuri (cha Kiroma), Kiodia, Kipijini cha Hawaii, na Kipomerania.
Ndugu Nicholas Ahladis, anayefanya kazi kwenye Idara ya Huduma za Tafsiri kwenye makao makuu, anaeleza hivi: “Habari iliyo katika machapisho yetu inawavutia watu wote ulimwenguni. Lakini baadhi ya vikundi vya utafsiri havina vifaa vingi, na huenda isiwezekane kwao kutafsiri kila toleo la Mnara wa Mlinzi. Halmashauri za Tawi zinazosimamia vikundi hivyo zinaweza kutuma ombi kwenye Halmashauri ya Uandikaji ya Baraza Linaloongoza zikipendekeza kwamba habari hususa itafsiriwe. Ilikuwa hivyo na toleo Na. 2 2021 la Mnara wa Mlinzi na ndiyo sababu lilitolewa katika lugha hizo hususa.”
Mambo yafuatayo yaliyoonwa katika lugha hizo yanakazia matokeo mazuri ya kampeni hiyo na jitihada zinazoendelea za kusambaza habari za Biblia kwa watu wa lugha zote.
Ni shangwe kubwa kwetu kujua kwamba gazeti Mnara wa Mlinzi liliwafikia watu wengi sana wakati wa kampeni hiyo ya pekee. Tunajua kwamba kampeni kama hizo zinaunga mkono mapenzi ya Mungu “kwamba watu wa namna zote waokolewe na kupata ujuzi sahihi wa kweli.”—1 Timotheo 2:4.