MACHI 5, 2020
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE
Ndugu Artem Gerasimov Ahukumiwa Katika Mahakama ya Crimea na Kutozwa Faini
Machi 3, 2020, Mahakama ya Jiji la Yalta ya Jamhuri ya Crimea ilimhukumu Ndugu Artem Gerasimov. Ingawa hatafungwa gerezani, mahakama imemtoza faini ya rubo 400,000 (au dola 6,000 hivi za Marekani). Atakata rufaa ya uamuzi huo.