Hamia kwenye habari

Ndugu Aleksandr Dubovenko na Ndugu Aleksandr Litvinyuk

DESEMBA 8, 2022
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE

Ndugu Dubovenko na Ndugu Litvinyuk Wahukumiwa Miaka Sita Gerezani

Ndugu Dubovenko na Ndugu Litvinyuk Wahukumiwa Miaka Sita Gerezani

Novemba 30, 2022, Mahakama ya Jiji la Armyanskiy iliyo katika Jamhuri ya Crimea iliwahukumu Ndugu Aleksandr Dubovenko na Ndugu Aleksandr Litvinyuk. Ndugu wote wawili walihukumiwa kifungo cha miaka sita gerezani na kupelekwa gerezani moja kwa moja.

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tunafarijiwa kujua kwamba sikuzote Yehova yuko kando yetu, popote tulipo na wakati wowote tunapokabili majaribu.​—Zaburi 139:7-12.

Mfuatano wa Matukio

  1. Agosti 2, 2021

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa. Ndugu wote wawili walishtakiwa kwa kutumia programu za kufanya mikutano kupitia video mtandaoni kuendeleza utendaji wa shirika lenye msimamo mkali

  2. Agosti 5, 2021

    Misako ilifanywa katika nyumba za familia nane za Mashahidi wa Yehova kutia ndani nyumba ya familia ya Dubovenko na ya Litvinyuk. Ndugu Litvinyuk alikamatwa na kupelekwa mahabusu

  3. Agosti 6, 2021

    Ndugu Litvinyuk aliachiliwa kutoka mahabusu na kuwekwa chini ya kifungo cha nyumbani

  4. Agosti 9, 2021

    Maofisa wa polisi walifanya tena msako katika nyumba ya Dubovenko. Aleksandr alihojiwa na kuwekwa chini ya kifungo cha nyumbani

  5. Agosti 11, 2021

    Ndugu Litvinyuk alishtakiwa rasmi kwamba alipanga utendaji wa shirika lenye msimamo mkali

  6. Februari 8, 2022

    Ndugu Dubovenko alishtakiwa rasmi kwamba alipanga utendaji wa shirika lenye msimamo mkali

  7. Aprili 29, 2022

    Kesi ya uhalifu ilianza. Hakimu alikataa ombi la Ndugu Litvinyuk la kumwona daktari na kupata matibabu alipokuwa chini ya kifungo cha nyumbani

  8. Septemba 8, 2022

    Ndugu wote wawili waliruhusiwa kuondoka nyumbani kila siku kati ya saa moja asubuhi na saa moja jioni

  9. Novemba 30, 2022

    Ndugu wote wawili walihukumiwa kifungo cha miaka sita gerezani

a b Maelezo ya kibinafsi yalitolewa kabla ya kuhukumiwa.