Hamia kwenye habari

MACHI 5, 2020
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE

Ndugu Sergey Filatov Ahukumiwa Katika Mahakama ya Crimea na Kupewa Kifungo cha Miaka Sita Gerezani

Ndugu Sergey Filatov Ahukumiwa Katika Mahakama ya Crimea na Kupewa Kifungo cha Miaka Sita Gerezani

Machi 5, 2020, Mahakama ya Wilaya ya Dzhankoysky ya Jamhuri ya Crimea ilimhukumu Ndugu Sergey Filatov. Amehukumiwa kifungo cha miaka sita gerezani. Ndugu Filatov ndiye Shahidi wa kwanza kuhukumiwa chini ya Sheria ya Uhalifu ya Urusi. Atakata rufaa ya uamuzi huo.