Hamia kwenye habari

Kukata miti ilikuwa mojawapo ya kazi zilizofanywa ili kuandaa eneo la Ramapo kwa ajili ya kazi ya ujenzi

NOVEMBA 8, 2024
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE

Mradi wa Makao Makuu wa Ramapo

Ujenzi wa Ramapo Waidhinishwa

Ujenzi wa Ramapo Waidhinishwa

Novemba 6, 2024, Kamati ya Mipango ya Mji wa Ramapo iliidhinisha ujenzi wa mradi wa Ramapo. Hatua hii muhimu inamaanisha kwamba sasa tunaweza kuanza ujenzi wenyewe.

Picha ya majengo yanayotarajiwa ya ofisi za Ramapo

Juni 2023, Kamati ya Mipango ya Mji wa Ramapo iliidhinisha baadhi ya mipango yetu ya ujenzi wa Ramapo. Hapo awali idhini kadhaa zilikuwa zimetolea kutia ndani idhini ya kukata miti. Hata hivyo, idhini hii ya sasa inaturuhusu kuanza kazi kama vile kujenga mwingilio na pia kupasua miamba na kuiondoa ili kujenga misingi ya majengo. Kazi nyingine kama vile kuchimba ardhini ili kuweka mabomba ya maji itaanza pia.

Ndugu Kevin Page, anayetumikia kwenye Halmashauri ya Mradi wa Ujenzi wa Ramapo, alisema hivi: “Sasa tuna idhini mkononi, tumefurahi sana! Katika kila hatua ya mradi huo, tumeona jinsi Yehova alivyobariki subira na kazi yetu ngumu. Tunamshukuru kwa kutusaidia kufikia hatua hii muhimu na tunasali kwamba aendelee kubariki kazi itakayofanywa katika hatua hii.”

Tukiwa undugu wa ulimwenguni pote, tumeguswa moyo na hatua hii ya hivi karibuni na tunasali Yehova aendelee kubariki mradi huu na wote watakaofanya kazi iliyo mbele yetu!—Hagai 1:14.