Hamia kwenye habari

Ndugu Artem Shabliy

APRILI 1, 2022
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE

Ulinzi wa Yehova Ni ‘Kama Ukuta wa Mawe’

Ulinzi wa Yehova Ni ‘Kama Ukuta wa Mawe’

Februari 16, 2022, Mahakama ya Jiji la Kerch ya Jamhuri ya Crimea ilimhukumu Ndugu Artem Shabliy na kumpa kifungo cha nje cha miaka miwili. Hahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Mfuatano wa Matukio

  1. Mei 26, 2020

    Maafisa wa usalama walipekua nyumba ya Artem na nyumba nyingine nne za Mashahidi wa Yehova nchini Crimea. Katika uvamizi huo, mwana wa Artem mwenye umri wa miaka minne alijeruhiwa miguuni kwa sababu wenye mamlaka walivunja kioo cha dirisha la nyumba yao. Baada ya upekuzi Artem alikamatwa na kuwekwa katika kifungo cha upweke kwa siku tatu

  2. Juni 9, 2020

    Artem aliiomba Mahakama ya Jiji la Kerch kumwonyesha ripoti za upelelezi uliofanywa unaohusiana na kesi inayomkabili. Licha ya kwamba ni haki yake kuona ripoti hiyo mahakama ilikataa ombi lake

  3. Mei 24, 2021

    Kesi yake ilianza kusikilizwa. Kulikuwa na ndugu na dada wengi mahakamani ambao walienda kumuunga mkono, lakini walikatazwa kuingia mahakamani

Maelezo Mafupi Kumhusu

Kama Artem alivyojionea, Yehova anaendelea kuwategemeza waabudu wake waaminifu kwa ushikamanifu. Tuna uhakika kwamba Yeye ataendelea kuwa jabali, ngome na kimbilio salama kwa ajili ya ndugu na dada wa Crimea na Urusi.​—Zaburi 18:2.