MEI 5, 2014
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE
Maoni ya Wataalamu Kuhusu Haki ya Kukataa Utumishi wa Kijeshi kwa Sababu ya Dhamiri
Wataalamu wa haki za kibinadamu wanazungumzia jinsi kukataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri kulivyokuja kuwa haki ya kibinadamu barani Ulaya.
Bw. Nils Muiznieks ni Kamishna wa Haki za Kibinadamu katika Baraza la Ulaya, ambaye amepewa mamlaka ya kuchunguza ikiwa nchi ambazo ni sehemu ya baraza hilo zinafuata haki za kibinadamu.
Bw. Richard Clayton QC ni mwakilishi wa Uingereza katika Tume ya Venice. Tume ya Venice ndiyo kamati inayolishauri Baraza la Ulaya kuhusiana na sheria za katiba.
Tazama mambo makuu ya mahojiano haya yenye kusisimua.