Hamia kwenye habari

NOVEMBA 29, 2018
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE

Maofisa Nchini Urusi Wavamia Nyumba Nane za Mashahidi Katika Eneo la Crimea

Maofisa Nchini Urusi Wavamia Nyumba Nane za Mashahidi Katika Eneo la Crimea

Alhamisi, Novemba 15, 2018, maofisa 200 wa Usalama wa Taifa (FSB) nchini Urusi walivamia nyumba nane za Mashahidi wa Yehova katika eneo la Crimea.

Kwa sababu ya mshtuko na mahangaiko yaliyotokana na kuvamiwa na maofisa wa FSB wenye silaha waliojifunika nyuso, Mashahidi wawili walilazimika kukimbizwa hospitalini kwa sababu shinikizo la damu liliongezeka sana. Pia, tunasikitika kuwaeleza kwamba mimba ya dada mmoja iliharibika.

Wakati wa uvamizi huo, maofisa walimtendea kwa jeuri Aleksandr Ursu mwenye umri wa miaka 78. Alibanwa ukutani, akalazimishwa kulala chini, na kufungwa pingu. Pia, polisi waliwahoji Mashahidi wengine.

Kwa sasa, Ndugu Sergey Filatov (kwenye picha kulia) ndiye peke yake aliyefunguliwa mashtaka ya uhalifu. Wenye mamlaka wamemshtaki chini ya Kifungu 282.2, sehemu ya 1, ya Sheria ya Uhalifu ya Urusi—sheria ambayo Shirikisho la Urusi imelazimisha ifuatwe na wakaaji wa rasi ya Crimea. Yeye ni baba wa watoto wanne, na ndiye Shahidi wa kwanza Crimea kukabili mashtaka chini ya sheria ya Urusi ya kukabiliana na msimamo mkali.

Ingawa tunahangaishwa na jinsi ndugu zetu wanavyovamiwa na kunyanyaswa, tunamtegemea Mungu wetu Yehova kwa ujasiri, kwamba atatuimarisha katika siku hizi za mwisho zenye majaribu mengi.—Isaya 41:10.