NOVEMBA 3, 2017
URENO
Moto Wenye Madhara Mengi Zaidi Katika Historia ya Ureno
Hali mbaya ya hewa iliyohusisha ukame mkali imechangia kuwe na msimu wenye moto hatari zaidi kurekodiwa nchini Ureno. Watu 64 walikufa mwezi wa Juni na wengine 45 mwezi wa Oktoba, kulikuwa na mikasa 523 ya kutokea kwa moto ambayo iliripotiwa mwezi wa Oktoba. Kulingana na European Union’s Emergency Management Service, mwaka huu tu moto wa msituni umeteketeza karibu ekari milioni 1.3—mara sita zaidi ya wastani wa kawaida nchini humo wa ekari 205,000.
Kulingana na ofisi ya tawi ya Ureno, moto huo umemwua ndugu yetu mmoja na mpwa wake wa miaka minne. Moto uliharibu au kuathiri nyumba za akina ndugu, pia uliathiri mashamba, vifaa, na kuua mifugo. Ndugu na dada wamejitahidi kusaidiana kufanya usafi baada ya uharibifu uliosababishwa na moto, wameondoa miti na takataka nyingine.
Halmashauri ya Kutoa Msaada imefanya kazi ya kuandaa msaada unaohitajiwa. Isitoshe, washiriki wawili wa Halmashauri ya Tawi nchini Ureno waliungana na waangalizi wa mzunguko na wazee kuwatembelea ndugu na dada ili kuwatia moyo.
Tunasali kwamba Yehova awategemeze kwa upendo na kuwafariji ndugu zetu nchini Ureno ili wapate nguvu tena baada ya uharibifu mkubwa uliosababishwa na moto.—Zaburi 71:21.
Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:
David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1-845-524-3000
Ureno: João Pedro Candeias, simu +351-214-604-339