Hamia kwenye habari

Urusi

 

2022-03-15

URUSI

Mashahidi wa Yehova Wanamuunga Mkono Ndugu Konstantin Bazhenov Wakati wa Kifungo Chake, Kuachiliwa, na Kufukuzwa Nchini

Konstantin Bazhenov ni mmoja kati ya Mashahidi wa Yehova nchini Urusi kukamilisha kifungo chake tangu marufuku iliyotangazwa na Mahakama Kuu mwaka wa 2017. Mei 5, 2021, baada ya kuwa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu, aliachiliwa mapema na muda mfupi baada ya hapo akafukuzwa nchini.